الصفحة الرئيسية » » SABABU 25 ZINAZOMFANYA MUISLAMU ASHEREHEKEE MAZAZI YA MTUME S.A.W:

SABABU 25 ZINAZOMFANYA MUISLAMU ASHEREHEKEE MAZAZI YA MTUME S.A.W:

SABABU 25 ZINAZOMFANYA MUISLAMU ASHEREHEKEE MAZAZI YA MTUME S.A.W:
1: Mawlid ni kuonesha kumfurahikia Mtume s.a.w, na kufurahikia mazazi ya Mtume s.a.w kulimnufaisha kafiri, jee sisi waislamu?! na hio ni dalili aloitumia Ibnu hajar katika fat7ul bary v9 p145 aliposema:
وذكر السهيلي أن العباس بن عبد المطلب رضي الله عنه قال : لما مات أبو لهب رأيته في منامي بعد حول في شر حال فقال ما لقيت بعدكم راحة الا أن العذاب يخفف عني كل يوم اثنين قال وذلك أن النبي صلى الله عليه وسلم ولد يوم الإثنين وكانت ثويبة بشرت أبا لهب بمولده فاعتقها .
Ametaja imam assuhayli kua Abbaas bin Abdilmuttwalib r.a.3 amesema: alipokufa Abu lahab nilimuona ndotoni baada ya mwaka yupo katika hali mbaya, akanambia sijapata baada yenu mapumziko, ispokua nakhafifishiwa adhabu kila siku ya jumatatu, akasema na jilo ni kwasababu Mtume s.a.w amezaliwa siku ya jumatatu na Thuwayba alienda kumpa bishara Abu lahab kwa kuzaliwa Mtume s.a.w akamwacha huru.
Ikiwa huyu kafiri aliefurahikia mazazi ya Mtume s.a.w mara moja kwa kumwacha huru kijakazi chake, anakhafifishiwa adhabu kila jumatatu, jee waislamu wanamfurahikia mara kwa mara watapata jaza gani kwa Allaah s.w.
2: Mtume s.a.w alikua akiitukuza siku ya kuzaliwa kwake na akiisherehekea kwa kufunga kama ilivothubutu katika hadithi iliopokewa na Imam Muslim kutoka kwa Abu Qatada kua Mtume s.a.w alipoulizwa kwanini anafunga jumatatu akasema ni siku nilozaliwa na kuteremshiwa wahyi.
عَنْ أَبِى قَتَادَةَ الأَنْصَارِىِّ رضى الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ -صلى الله عليه وسلم- سُئِلَ عَنْ صَوْمِ الاِثْنَيْنِ فَقَالَ ( فِيهِ وُلِدْتُ وَفِيهِ أُنْزِلَ عَلَىَّ) .
3: Tumeambiwa na Allaah s.w katika Qur'an tumfurahikie Mtume s.a.w:
. ( قُلْ بِفَضْلِ اللَّهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَبِذَلِكَ فَلْيَفْرَحُوا هُوَ خَيْرٌ مِمَّا يَجْمَعُونَ )) (يونس:58)
Sema kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake, basi na wafurahi kwa hayo, haya ni bora kuliko hayo wanayo yakusanya.
Katika aya hii Mwenyezi Mungu s.w anatuamrisha kuifurahikia rahma, na Mtume s.a.w ndio rahma adhimu. Asema Mwenyezi Mungu s.w katika aya nyengine: ( وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلاَّ رَحْمَةً لِلْعَالَمِينَ )) (الانبياء:107))
Na hatukukutuma ispokua ni rehema kwa walimwengu.
4: Mtume s.a.w alikua akizingatia mafungamano kati ya zama na matokeo ya kidini yalopita, inapofika wakati ambao lilitokea ndani yake lile tokeo hua ni farsa na kulikumbuka, na kuitukuza siku hio, kwasababu ya hilo tukio. Na huu msingi ameuweka mwenyewe Mtume s.a.w kama ilivokuja kwa Bukhary na Muslim na Tirmidhy na wengineo kua Mtume s.a.w alipofika madina alikuta mayahudi wakifunga siku ya ashuraa, akaulizia kuhusu hilo, akaambiwa: kwamba wanaifunga kwasababu Mwenyezi Mungu amemuokoa Mtume wao na akamzamisha adui wao katika siku hii, kwahivo wao wanaifunga kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema hio, Mtume s.a.w akasema: sisi ni bora kumkumbuka Musa kuliko nyinyi, akafunga na akaamrisha watu wafunge.
Alhafidh Ibn Hajar ndio mwanachuoni wakwanza kutolea dalili hadithi hii katika kufaa kufanya mawlid... na hakuna muislamu anaeshuku aqida ya Ibn Hajar, na maulamaa wote wamekubaliana kua yeye ndie amiri wa waumini katika hadithi.
5: Mawlid yakupelekea kumswalia Mtume s.a.w, na Mwenyezi Mungu s.w ametuamrisha kumswalia aliposema:
. ( إِنَّ اللَّهَ وَمَلائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيماً )) (الأحزاب:56)
Na chochote kinachokupelekea kufanya yaloamrishwa na sheria basi kitu hicho pia kinakubalika kisheria, kwani kumswalia Mtume s.aw kunamfaidisha mja mambo mengi:
A: Anakua amefwata amri ya Mwenyezi Mungu s.w.
B: Anaswaliwa na Mwenyezi Mungu s.w mara kumi kwa swala moja.
C: Anapandishwa daraja kumi na kuandikiwa thawabu kumi na kufutiwa madhambi kumi.
D: Mtume s.a.w humrudishia salamu.
E: Huondolewa hamu zake na kusamehewa madhambi yake... Na mengine mengi...
6: Mawlid yamekusanya kutaja mazazi yake na sera yake na miujiza yake, na sisi waislamu tumeamrishwa kumjua Mtume s.a.w na kumfuata, tunapohudhuria mawlid tunapata kuyajua yote hayo.
7: Unapomsifu Mtume s.a.w unapata jaza kutoka kwake, kama alivokua akiwajazi washairi walokua wakimsifu, alimpa Ka'b bin Zuhayr kishale na akatengezea Hassaan bin thabit membar. Na alikua akifurahikia kusifiwa, vipi asiurahikie kwa kukusanywa sera yake na sifa zake na miujiza yake!!!
Ametaja Alhafidh ibn Sayyidin naas katika kitabu cha منح المدح zaidi ya maswahaba mia moja na sabiini walomsifu Mtume s.a.w kwa mashairi mazuri mazuri.
8: Maswahaba hawakuwacha kumsifu Mtume s.a.w hata baada ya kufa, tena ndani ya msikiti. ametaja Imam shafi katika musnad yake (1706), wakati wa khilafa ya sayyidna Omar r.a.3 aliingia msikitini akampata Hassan bin thabit akitoa mashairi ya kumsifu Mtume s.a.w, akamwambia: Hassan watoa mashairi katika msikiti wa Mtume s.a.w?!!! Hassaan akamjibu: nimeyatoa mbele ya ambae ni mbora kuliko wewe ewe Omar, akamgeukia Abu hurayra r.a.3 akamwambia: hukumsikia Mtume s.a.w akisema: ewe Mola mjaalie Jibril amuunge? Abu Hurayra akasema: ndio nimemsikia. akasema: wakamwekea membar Hassaan msikitini ili atoe mashairi ya kumsifu Mtume s.a.w.
Hii ni dalili tosha kuonesha maswahaba walimsifu hata baada ya kufariki, na maneno ya Sayyidna Omar r.a.3 hayakua kwa ajili ya mashairi au kumsifu Mtume s.a.w, bali yalikua kwa ajili ya sehemu ambayo ni msikiti, lakini alipojua kua wakati wa Mtume s.a.w alikua akiyatoa msikitini mbele ya Mtume s.a.w akajua inafaa na akamwekea na membar khaswa kwa hilo.
9: Kujua miujiza yake na sera yake na tabia zake Mtume s.a.w kwazidisha imani kwake na kwa aliemtuma, kwani mwanadamu ameumbwa kupenda mazuri ya umbo, tabia, ilimu, amali na mengineyo, na hakuna tabia nzuri na zilokamilka na bora kama za Mtume s.a.w... na kuongeza mahaba inatakikana katika sheria, kwahivo na lolote lenye kupelekea hilo pia latakikana.
10: Kumtukuza Mtume s.a.w ni jambo liloamrishwa katika sheria,
. ( 9 : لتؤمنوا بالله ورسوله وتعزروه وتوقروه وتسبحوه بكرة وأصيلا ) (سورة الفتح)
Na kufurahikia siku ya kuzawa kwake kwa kudhihirisha furaha na kukusanyika kuleta dhikri, na kuweka chakula, na kuwakirimu maskini ni katika alama za kumtukuza na kumfurahikia na kumshuru Mwenyezi Mungu s.w. kwa kutuongoza kwa dini ya kiislamu na kutuletea zawadi kubwa ambayo ni Mtume s.a.w.
11: Mtume s.a.w alipokua anataja ubora wa siku ya ijumaa alitaja kua ni siku aloumbwa nabii Adam a.s, ikiwa ijumaa imekua bora kwa kuumbwa nabii Adam siku hiyo, jee siku alozaliwa mbora wa Mitume na manabii itakosaje kua ni siku bora!!!
12: Qur'an imetaja mazazi ya baadhi ya mitume, na hii ni dalili tosha kuonesha siku ya mazazi ya Mtume s.a.w ni siku tukufu na ni siku ya kukumbukwa.
13: Mtume s.a.w alipokua anaenda israa alipofika bayt lahm aliambiwa na Jibryl ashuke aswali rakaa mbili, alipomuuliza hapa ni wapi, akamwambia hapa ni sehemu alipozaliwa nabii Isa a.s. IKiwa sehemu alozaliwa nabii Isa a.s imestahiki kukumbukwa, vipi mazazi ya Mtume s.a.w yasikumbukwe!!!
14: Mwenyezi Mungu s.w katika Qur'an anasema:
. ( وَكُلاًّ نَقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنْبَاءِ الرُّسُلِ مَا نُثَبِّتُ بِهِ فُؤَادَكَ )) (هود: من الآية120)(
Na yote tunayo kusimulia katika khabari za Mitume ni ya kukupa nguvu moyo wako.
Ikiwa moyo wa Mtume s.a.w wapewa nguvu kwa kusimuliwa khabari za Mitume, jee sisi hatustahiki kuzipa nyoyo zetu nguvu na thabati kwa kusimuliana khabari za Mtume s.a.w?!!!
15: Kuhuisha ukumbusho wa mazazi ya Mtume s.a.w ni kitu kinacho takikana kisheria, kwani hatuoni amali za hajj nyingi ni kuhuisha ukumbusho ulotangulia, kama kupiga mawe jamaraat na sa3y kati ya swafa na marwa na kuchinja katika mina.
16: Amepokea Imam bayhaqi kutoka kwa Anas r.a.3 kua Mtume s.a.w alijichinjia aqiqa baada ya kutumilizwa. Na imepokewa kua babu yake alimchinjia siku ya saba baada ya kuzaliwa. Imam Suyuti asema: na aqiqa hua ni mara moja tu, itakua maana ya kitendo hicho ni kua alichokifanya Mtume s.a.w ni kudhihirisha shukurani kwa kuletwa na Mwenyezi Mungu kama rahma kwa walimwengu, kwahivo inapendekezwa kudhihirisha shukurani kwa kuzawa kwake na kulisha chakula na mengineo katika sampuli za ibada na furaha.
17: Mwenyezi Mungu s.w katika Qur'an asema:
. ( اللَّهُمَّ رَبَّنَا أَنْزِلْ عَلَيْنَا مَائِدَةً مِنَ السَّمَاءِ تَكُونُ لَنَا عِيداً لِأَوَّلِنَا وَآخِرِنَا وَآيَةً مِنْكَ وَارْزُقْنَا وَأَنْتَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ ) المائدة / 114 )
Ewe Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wetu! Tuteremshia chakula kutoka mbinguni ili kiwe Sikukuu kwa ajili ya wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu, na kiwe ni Ishara itokayo kwako. Basi turuzuku, kwani Wewe ndiye mbora wa wanao ruzuku.
Ikiwa kuteremshwa meza ya chakula waliifanya ni sikukuu ya kuikumbuka hio neema, jee siku ya kuzaliwa neema kubwa (Mtume s.a.w) si inastahiki zaidi kukumbukwa!!!
18: Mwenyezi Mungu s.w katika Qur'an anaamrisha kukubusha masiku yake Mwenyezi Mungu s.w:
. ( وَذَكِّرْهُمْ بِأَيَّامِ اللَّهِ ...) (إبراهيم:5)
Na uwakumbushe siku za Mwenyezi Mungu.
Jee kuzaliwa kiumbe bora na rehema ya walimwengu na Mtume wa mwisho sio siku katika masiku ya Mwenyezi Mungu? siku ambayo imepelekea kupatikana Mtume alikuja kuziongoza nyoyo na kuwatoa watu katika kiza cha ushirikina na ukafiri.
19: Mawlid ni moja katika njia ya kufanya da'wa, na sote tunakubali kua mawlid imesilimisha malaki ya watu afrika mashariki, hii ni dalili tosha kuonesha ni jambo la kheri.
20: Amenukuu sheikh Ibn taymiya katika iqtidhwaa kurasa ya 304 na 305 kua maansari kabla ya kuja Mtume s.a.w madina walisema: tuangalieni siku tukusanyike tukumbuke hii neema alotuneemesha Mwenyezi Mungu s.w, wakasema: siku ya jumamosi, kisha wakasema: hatutangamani na mayahudi katika siku yao, wakasema jumapili, wakasema: hatutangamani na manaswara katika siku yao, wakasema ijumaa, wakajumuika katika nyumba ya Abu umamah Sa3ad bin Zurarah, wakachinjiwa mbuzi akawatosha wote.
21: Mawlid imefanywa kwa mda ma maqarne bila ya kupingwa na wanazuoni, na wametaja sherehe ya mawlid wana tarekhe katika vitabu vyao, kama Ibnu kathyr na Ibnul jawzy na Ibnu dihya al'andalusy, na Ibnu hajar na Assuyutwy na wengineo. na wote hao ni vigogo katika elimu.
Ha hadithi ya ibn mas'ud yasema:
. "مَا رَآهُ المُسلِمونَ حَسَناً فَهوَ عِندَ اللهِ حسنٌ، وَمَا رَآهُ المُسلمونَ قَبيحاً فَهوَ عندَ اللهِ قَبيحٌ"
Wanaloliona waislamu ni jema basi na mwa Mwenyezi Mungu pia ni jema, na wanachokiona waislamu ni kiovu basi na kwa mwenyezi Mungu pia ni kiovu.
22: Mwenyezi Mungu s.a.w asema:
{وَمَنْ يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّهِ فَإِنَّهَا مِنْ تَقْوَى الْقُلُوبِ} [الحج:32]
Na mwenye kutukuza sha'air za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo.
Ikiwa kuadhimisha na kutukuza tambiko la Mwenyezi Mungu s.w ni katika unyenyekevu wa nyoyo, basi na Mtume s.a.w ni tambiko la Mwenyezi Mungu s.w, na kutukuza mazazi yake ni kumtukuza yeye.
23: Kuhudhuria mawlid kunakuza mahaba ya mu'min kwa Mtume s.a.w, na Mtume s.a.w anasema katika hadithi iliopokewa na Imam Bukhary:
. "لاَ يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى أَكونَ أحبَّ إليه مِن والده وَوَلدِه وَالنَّاسِ أَجمعين"
Haikamiliki imani ya mmoja wenu mpaka anipende mimi zaidi ya mzazi wake na watoto wake na watu wote.
24: Maulamaa wakubwa walofika daraja ya kua mahuffaadh wametunga vitabu kuhusu mawlid:
A: Alhaafidh ibnu kathyr. Ametaja hilo Ibn hajar katika addurarul kaaminah.
B: Alhafidh al'iraqy, ametunga : المورد الهني في المولد السني .
C: Alhaafidh Ibn naaswiruddyn addimashqy, huyu ana vitabu vitatu:
1: جامع الآثار في مولد النبي المختار
2: اللفظ الرائق في مولد خير الخلائق
3: مورد الصادي في مولد الهادي .
D: Alhaafidh Assakhaawy, ametunga: الفخر العلوي في المولد النبوي .
E: Alhaafidh Mullaa Ali Alqaary, ametunga: المورد الروي في المولد النبوي .
F: Alhaafidh Ash'shaybany Azzabidy, anaejulikana kwa Ibnud dayba3, ametunga maulidi yake mashuhuri mawlid addayba3.
G: Alhaafidh Assuyutwi, ametunga حسن المقصد في عمل المولد .
H: Alhaafidh ibnu Dihya, ametunga: التنوير في مولد البشير النذير .
J: Alhaafidh Ibnul jazary, ametunga: عرف التعريف بالمولد الشريف .
Mbali na hufaadh kuna muhadditheen walotunga mawlid na fuqahaa na mufassireen na wengineo wengi, hatutowataja wote kwa kutorefusha nukta hii.
25: Sababu wanazotoa wanaokata kusherehekea mawlid:
1: wanasema lingekua ni kheri basi Mtume s.a.w angelifanya!
Tunawauliza: jee kutia nukta na shakli katika msahafu ni kheri ama si kheri? na Mtume s.a.w hakulifanya, jee tuzitoe kwa kua Mtume s.a.w hakulifanya?
2: wanasema Mtume s.a.w hakufanya mawlid!
Sio kila ambalo hakuliamrisha Mtume s.a.w wala hakulikataza halifai, mashindano ya Qur'an Mtume s.a.w hakuyafanya, tahajjud kwa jamaa msikitini Mtume s.a.w hakuifanya, kukhitimisha msahafu katika tarawehe Mtume s.a.w hakulifanya, na nyiyi mnaopinga mawlid mwayafanya yote hayo na hayakufanywa na Mtume s.a.w.
3: wanasema Mtume s.a.w amesema mwenye kuzusha katika dini kisokua katika dini basi haikubaliwi!
Tunawaambia hamukuifahamu hadithi kama walovyoifahamu maulamaa, Mtume s.a.w amesema kisokua katika dini, ama kilioko katika dini basi kinakubaliwa, na yote yanayopatikana katika mawlid kama kusoma Qur'an na kumswalia Mtume s.a.w na kulisha chakula yote yapo katika dini.
4: wanasema kufanya mawlid ni kumtuhumu Mtume s.a.w kua amefanya khiyana na haitufikishia kila jambo katika dini!
Tunawaambia na hayo mambo tulowatajia hapo juu ambayo munayafanya nyinyi na hayakutajwa na Mtume s.a.w sio kumtuhumu kwa khiyana? kisha maulamaa waloweka mambo haya tayari mushawatuhumu.
5: wanasema katika baadhi ya mawlidi kunapatikana munkarati, kwahivo ni haramu!
Kwanza twawauliza, jee isokua na munkaraati mwaikubali? pili kama kuweko munkaraati kwa baadhi ya mambo itapelekea kuharamisha yote basi itabidi tuharamishe harusi pia, maana kuna zengine hujaa munkarati.
6: wanasema mawlidi haifai kwasababu kwasifiwa Mtume s.a.w sana, na Mtume s.a.w amekataza aliposema:
. "لا تُطْروني كما أطْرَتِ النَّصارى الْمَسيحَ ابنَ مَرْيَمَ"
Tunawaambia neno itraa katika lugha maana yake ni kuvuka mpaka katika kusifu, na kuvuka mpaka kwenyewe tayari Mtume s.a.w amekupigia mfano katika hadithi hiohio aliposema kama walivyo vuka mpaka manaswara kwa Isa... ni mpaka upi huo waliovuka manaswara? walifika kumuita Mungu na Mtoto wa Mungu!!! jee kuna muislamu ambae anaitakidi Mtume s.a.w ni Mungu ama ni mtoto wa Mungu?
Kwahivo namna tutakavyo msifu madamu hatujafika katika huo mpaka basi hakuna uharamu wala makosa.
Na qaa3ida ya kiusuli yasema, kukatazwa kitu ni kuamrishwa kinyume chake, kwahivo Mtume s.a.w katika hadithi hii hajatukataza kumsifu sana, bali ametuamrisha kumsifu sana, madamu hatutavuka mipaka.
7: wanasema kufanya mawlid ni kuyafunga mahaba ya Mtume s.a.w katika siku moja tu!
Tunawauliza: pale Mtume s.a.w aliposema sisi ni awla kumsherehekea Musa kuliko wao, kisha akafunga na akaamrisha watu wafunge, jee aliyafunga mahaba ya nabii Musa katika siku moja?!!!
8: wanasema maswahaba walikua ni wabora na wanampenda Mtume s.a.w kuliko sisi na hawakunya mawlid!
Tunawaambia jee alotia nukta katika msahafu wakati wa Hajjaaj bin Yusuf alikua aipenda Qur'an kuliko maswahaba? jee Sayyidna Omar r.a.3 alipowakusanya watu msikitini kuswali tarawehe alikua ni mbora kuliko Sayyiduna Abu bakr ambae hakulifanya hilo? jee sayyiduna Uthmaan r.a.3 alipoweka adhana yapili alikua ni mbora kuliko sayyidna Abu bakr na sayyidna Omar? wanazuoni wamesema: الْمَزِيَّةُ لا تَقْتَضي التَّفْضيلَ .
9: wanasema mawlid imekua ni hoja ya wanaoenda kufanya uchafu wao!
Tunawaambia tatizo lipo katika nia ya huyo mtu, wala sio kwa mawlid, na kama anavotumia mawlid kama hoja na pia atatumia mengine pia kama kuenda tarawehe... kuna watu wanaenda hajj kwa ajili ya kuiba, na wengine huenda kutongoza na wengine huenda kufanya makubwa kushinda hayo, jee tuondoe ibada ya hajj? usiseme huswali kwa kua nguo ina najasa, safisha najasa uswali.
10: wanasema mawlid ni katika mambo yenye shaka, na Mtume s.a.w ametuambia tuwache yenye shaka!
Tunawaambia shaka ipo katika wahm zenu, ama kwetu hamna shaka hata kidogo kua mawlid yafaa na hayapingani na mafundisho ya dini.
Mwisho : nasiha kwa wanaotumia juhudi kubwa kupinga mawlid: lau mungutumia juhudi hizo katika kukataza mambo ya haramu ambayo hayana shaka tungekua hatuna uchafu tunaouona katika jamii, kuenea madawa ya kulevya na zinaa na vijana kupuuza swala na mengineo.

0 التعليقات:

إرسال تعليق