Sambo ya
kiwandeo ni shairi kwa bahari ya utendi "utenzi"( shairi ndefu leny mishororo minne
kila ubeti na mshororo haugawanywa na vipande.) ,mtungaji
wake ni Ahmed Sheikh Nabahany na Ahmed Sheikh Nabahany ni moja wa washairi
wakubwa katika Kiswahili na moja wa mwongozi wa mtendo wa urasimi
mpya,alizaliwa tarehe 27 mwezi novemba mwaka 1927 BK wazazi wake walikufa
wakati wa utoto wake na alilewa na nyanya wake Amina Abubakr Sheikh , na bibi
huyu ni mshairi maarufu sana na moja kwa ushairi wake ni utendi wa "Ngamia
na paa ", na Ahmed Sheikh Nabahany alirithi kipaji hicho kutoka nyanya
wake na kutoka mashairi yake mashuri sana ni " Sifa za mnazi" yenye
beti 79 na "Manukato ya wambedja" yenye beti 107,pamoja na Sambo ya
kiwandeo.
Bahari ya
utenzi wa sambo ya kiwandeo iliundwa kwa silabi /ya/. Utenzi huo una beti 217.utenzi
una mishororo minne ,urari wa mizani katika kila mshororo ni mizani nane,
mishororo mitatu ya kwanza ina kina kimoja ,na kina cha kituo (mshororo ya
mwisho) ni kina cha bahari kilichokaririwa mwishoni mwa kituo katika kila ubeti
hadi mwisho yaani ni bahari ya mtiririko. Utenzi ulitungwa kwa lahaja ya kiamu
na kimvita .kiamu hasa kizingatiwa kama lahaja ya ushairi . Mshairi alitumia baadhi
ya maneno kutokana lugha ya kiarabu lakini kwa matamshi ya kiswahili (Utohozi),
pamoja na tamathali ya usemi na mbinu ya lugha kama sitiari,tashbiha, na
hasahasa taswira,n.k
Anuani ya utendi ni sambo ya kiwandeo na kiwa ndeo
ni kisiwa cha lamu na sambo ni jina la jahazi kubwa liliundwa zamani kale
wakati wa mtume maarufu sana Nuhu (A.S). sambo iliandikwa na lahaja ya kiamu maudhui
yake ni kueleza hali ya watu walioishi pwani hasa mjini lamu na ujuzi wao
baharini hasa hasa kwenye kujenga jahazi na mtepe bela ya kutumia misumari
lakini ubao ulifungwa na mwingine kwa kamba maalumu , sambo hii ni jahazi kubwa
katika zama ya mtume Nuhu (A.S) , Baada ya kueleza namna ya kuundwa kwa jahazi
na kusifu sehemu jahazini na namna ya kuitengeneza, Sheikh Nabahany alieleza hali ya vipi jahazi kusafirishwa ili
kuchukua bidhaa na waabiria kupita nchi mbalimbali kama Msumbiji , Bukini, Bara
laArabu, na Bara la Hindi.
Utenzi
ulitungwa tarehe 18 mwezi aprili mwaka 1970 BK kama ilitajwa ubeti 214 ili
kusajili na kuhifadhi sira ya jahazi hili kutoka mzizi hadi mwingine kama
ilivyotajwa katika ubeti 208 hii ni dhamira ya utenzi.
0 التعليقات:
إرسال تعليق