الصفحة الرئيسية » » قصيدة رثاء الأستاذ اسماعيل مفاومى تأليف أحمد خلف

قصيدة رثاء الأستاذ اسماعيل مفاومى تأليف أحمد خلف



Mfaume, Mfalume, Mfalme
Mtu mwenye rehema,
Tabia yake ni njema,
Moyo wake ni mwema.
Mfaume, Mfalume, Mfalme
Je yeye ni mfalme?
Ni mfalme.
                                           Si mfalme.
Ni mfalme.
                                           Si mfalme.
Ndiyo,yeye ni  kiongozi wa wafalme.
Je, ana mamlaka?
Ana mamlaka.
                                               Hana mamlaka.
Ana mamlaka.
                                               Hana mamlaka.
Ndiyo, ana mamlaka kwa yake ufalme.
Iko wapi yake mamlaka?
Nyoyo zetu ni yake mamlaka,
Mahaba yetu ni yake mamlaka,
Amali njema ni yake mamlaka,
sera bora  ni  yake  mamlaka.
Mfaume, mfalume, mfalme.
Bwana mfaume ni wetu mfalme.
Kwa heri bwana mfaume,
Iwe na sahaba ya mtume,
Iwe na ridha ya mfalme,
Mwenyezi Mungu mfalme wa wafalme.
Kwa heri bwana mfaume,
Kwa heri mfaume, mfalume, mfalme

0 التعليقات:

إرسال تعليق