الصفحة الرئيسية » » قصيدة من تاليف أحمد خلف

قصيدة من تاليف أحمد خلف



Tutaweza pamoja pamoja
Uwezekano ni kitu kigumu
Mashaka nyingi iliyomo
Tushike ushirikiano na azimo
Tutaweza pamoja pamoja
Mtu moja mohala hawezi
Kufanya hata moja kazi
Hata wanyama wa kizizi
Wanashirikiana katika zizi
Tutaweza pamoja pamoja
Ushirikiano katika Quraani
Ni wasia ya Manani
Ni njia kupata jinani
Tushirikiana katika ihsani
Tutaweza pamoja pamoja,
Mtu ambaye hashirikiani
Ni mawindo wa shitani
Kama mbuzi pweke njiani,
Tutaweza pamoja pamoja
Mshikeni  yangu wasia
Kwa nyoyo zilizotulia
Ushirikiano siri ya dunia
Hatinafsi ni binadamu hatia
Tutaweza pamoja pamoja
قصيدة من تأليف الفقير إلى الله أحمد خلف أبوالفضل

0 التعليقات:

إرسال تعليق