Alaa Jumamosi ni idi yake
halahala
Na Ahmed Khalaf
Tarehe: 6/4/2015
Alaa ibn Salah alitimia yake risala
Alimaliza uzamili kwa auni Mola
Alitafitia riwaya wakati yake na pahala
Kulinganishia Kiamhari na Kiswahili ala-ala
Hongera nasi rafiki zake
Mabruki Zaidi kazi zake
Baraka iwe milele mwenzake
Manufaa yapatanishe kutoka kwake
Alaa ibn Salah ili kusifu yake hala
Hatoshi kasida moja au hata makala
Sifa yake nzuri zilijaza ulimwenguni ghala
Tabasamu haimfariki wakati wowote au pahala
Bashasha usoni kwake
Mahaba ndani yake
Ujuzi bongoni mwake
Uzuri ndimini kwake
Alaa ibn Salah siku yake ni mahafala
Kasida hawezi kusifu yake jamala
Mwenyezi atusaidie kurudia yake tajamala
Alaa ibn Salah Jumamosi ni idi yake halahala



0 التعليقات:
إرسال تعليق